Dk Shoo awataka wakristo kujijengea ujasiri

  • Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dk Frederick Shoo, amewataka Wakristo kuwa wajasiri na wathubutu wa kukemea na kuonya  pindi yanapotokea maovu na matendo yasiyofaa katika jamii.
Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, amesema leo Aprili 8 kwamba  anatamani kungekuwa na Wakristo wengi wenye sauti na ujasiri  wa kukemea na kuonya kwa kusema ndugu yangu  Mwogope Mungu.
Shoo ameyasema hayo jana wakati akihubiri kwenye ibada ya Jumapili katika usharika wa Msaranga Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo  ambayo imetanguliwa  na Ufunguzi wa Nyumba ya Mtumishi, Uzinduzi wa mashine ya kusaga na kukoboa  pamoja na upandaji Miti.
Dk.Shoo amesema  katika dunia ya leo yenye watu wenye midomo michafu, unafiki mkubwa, kiburi, wenye kukata tamaa,  wanaokataa maonyo,  wasioona madhaifu yao na wasiotaka kutubu, kunahitajika wakristo ambao watasimama na kutubutu kusema Ndugu yangu mwogope Mungu.
Aidha Dk.Shoo amesema , Dunia inahitaji ushuhuda wa matendo mema, hivyo wakristo wanapaswa kusimama imara na kuwa na ujasiri wa kuonya na kuwaambia watu wamwogope Mungu.
"Ndugu zangu Mungu anataka kuwatumia  kutangaza ukuu wake, na natamani leo, kungekuwa na Wakristo wengi wenye sauti,inayoweza  kusema ndugu yangu mwogope Mungu"amesema Dk Shoo
Aidha amesema   anatamani pia kuwa na wakristo wenye ujasiri na ambao wanakaa na kuishi kwa upendo, amani na maelewano na binadamu wenzao bila ya kujali tofauti zao,ukabila,rangi au vyeo vyao.
"Yesu anatafuta mtu wa kumtuma katika jamii akaubiri na akaishi amani,upendo,maelewano na Haki, sasa wakristo tukubali kutumwa kwenda kushuhudia mahali popote".
Amesema  katika dunia ya leo kuna watu ambao wanajua kupanga maneno ambayo wanaweza kusema wanahubiri habari  za Yesu lakini maisha na mienendo yao ni kinyume na hayana uhalisia na Mungu wanayemtaja.
Shoo pia amewataka  wananchi kutunza na kuyalinda mazingira,hatua ambayo itasaidia kuwepo kwa maji ya kutosha katika vyanzo na kuepusha kuwepo kwa tatizo la upungufu wa maji.
Ibada hiyo mbali na Askofu, pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, Mwekahazina wa Dayosisi Exaudi Makyao, Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati, Kenedi Kisanga, pamoja na wachungaji mbalimbali na viongozi wa Serikali.

Download App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: