Jenerali ulimwengu:Tunatakiwa kuwauliza wenye madaraka; utamaduni wa kuhoji unaanzia nyumbani


Mwanahabari Mkongwe, Jenerali Ulimwengu amesema ukandamizwaji wa demokrasia nchini unasababishwa na hofu ya wananchi kuwahoji viongozi wao, huku akitaka kujengwa kwa jamii inayohoji tangu ngazi ya familia hadi Taifa.
Ulimwengu ameyasema hayo Aprili 13, katika mkutano wa 10 wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ulimwengu aliwataka wananchi kutokubali mambo kirahisi bali wawe wadadisi.
“Ndio maana tunatakiwa kuwauliza wenye madaraka, kwa mtu anayeongoza, nani amekupa mamlaka ya kusema hakuna maandamano ya kisiasa? Au unasema hakuna kufanya mkutano kwenye mkoa huu kwa sababu huishi hapa?” Amehoji Ulimwengu.
Ameongeza: “Nani aliyekwambia kwamba tukishamaliza uchaguzi na ikiwa umeshinda hakutakuwa na kampeni za siasa hadi uchaguzi mwingine ufike? Haya yote ni madaraka waliyojipa watu, wamejilimbikizia na kwa sababu hatuulizi kikamilifu, wanafikiri wako sawa.”
Ulimwengu ametaka kujengwa kwa jamii inayouliza maswali tangu ngazi ya familia na kuwataka wazazi kuwaruhusu watoto kuwauliza maswali.  
“Utamaduni wa kuhoji unaanzia nyumbani, waacheni watoto wawaulize maswali na muwe tayari kuwasikiliza. Wale wenye wajukuu nao waulize maswali. Kwa hiyo tuanzie kwenye nyumba zetu, vijijini na mitaani, tujenge jamii ya watu wasiochukulia vitu kiurahisi, bali wanauliza kila kitu,” amesema Ulimwengu.


Download App Yetu hapa chini, Bonyeza picha:-



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: