Makamishna wa tume ya uchaguzi Kenya wajiuzulu

Paul Kurgat (kushoto) Margaret Mwachanya (kati) na Consolata Nkatha - makimishna wa IEBC wamejiuzulu
Maafisa watatu wakuu wa tume ya uchaguzi nchini Kenya (IEBC) akiwemo naibu mwenyekiti wamejiuzulu wakidai kutokuwa na imani na mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati.
Makamishna hao wamedai kuwa bodi hiyo imeshindwa kutimiza wajibu na imeeingiliwa na watu wengine.
Wakihutubia wanahabari jijini Nairobi, makamishna hao Consolata Nkatha, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya wamedai kuwa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ameshindwa kuiongoza tume hiyo na kudai kwamba tume hiyo imeingiliwa na watu kutoka nje wanaoshawishi jinsi inavyofanya kazi.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula ChebukatiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati
''Kwa muda murefu sasa, mwenyekiti ameshindwa kutoa muongozo wa utaratibu kwa wakati mgumu na anapohitajika kufanya hivo.
Katika taarifa yake hivi punde kwa waandishi wa habari, mwenyekiti wa tume hiyo ya IEBC - Wafula Chebukati amesema kwamba hakujakuwa na mawasiliano rasmi kuhusu kujiuzulu kwa makamishna hao watatu na kwamba amepata kusikia kuhusu taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari nchini.
Badala yake, chini ya uongozi wake, bodi ya tume imegeuzwa kuwa sehemu ya kusambaza habari zisizo sahihi, kukuza kutoaminiana na kutengeneza nafasi ya kung'angania sifa.
Kutokana na hilo, tunajutia kutangaza kujiuzulu kutoka kwa tume mara moja.'' amesema Margaret Mwachanya, Kamishna wa IEBC.
Margaret Mwachanya, Kamishna wa IEBC (kushoto)
Image captionMargaret Mwachanya, Kamishna wa IEBC (kushoto)
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati katika ujumbe kwa vyombo vya habari amekana kujulishwa kuhusu uamuzi wa makamishna hao na kudai alipata habari kupitia vyombo vya habari .
Uamuzi wa kujiuzulu kwao unajiri wiki moja tu baada ya mwenyekiti Wafula Chebukati kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji Ezra Chiloba kutokana na madai ya kuhusika na kashfa ya ununuzi wa baadhi ya vifaa vya utendaji kazi katika tume hiyo.
Rosyln Akombe Kamishna wa tume ya IEBC aliyejiuzulu 2017 akidai kuwa tume haina uwezo ya kuandaa uchaguzi huru na wa haki
Image captionRosyln Akombe Kamishna wa tume ya IEBC aliyejiuzulu 2017 akidai kuwa tume haina uwezo ya kuandaa uchaguzi huru na wa haki

Kujiuzulu kwa makimishna wa IEBC ina maana gani?

Tume hiyo ya makamishna saba sasa imesalia na watatu tu baada watatu kuondoka hii leo.
Kwa jumla makamishna waliondoka ni zaidi ya nusu.
Kuondoka kwao sasa kunaacha tume hiyo bila idadi ya makamishna inayohitajika kisheria kutimiza wajibu wake hadi ivunjiliwe mbali na tume mpya kuundwa.
Tume hiyo imekumbwa na msukosuko na kujiwekea rekodi ya aina yake.
Mahakama ya juu zaidi ilifutilia mbali uchaguzi uliyosimamiwa na tume hiyo.
Uhuru Kenyatta (lkushoto) alitangazwa kumshinda Raila Odinga katika uchaguzi wa marudio 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionUhuru Kenyatta (lkushoto) alitangazwa kumshinda Raila Odinga katika uchaguzi wa marudio 2017
Kisha upinzani nchini Kenya ukiongozwa na kinara Raila Odinga ukaususia uchaguzi wa marudio ukitaka tume hiyo kuvunjiliwa mbali.
Hilo halikufanyika na rais Uhuru Kenyatta akatangazwa mshindi wa kura hizo kwa asilimia kubwa.
Hata hivyo upinzani ulizidi kushikilia tume hiyo ivunjwe hata baada ya uchaguzi lakini serikali ikapinga.
Kujiuzulu kwa makamishna hao sasa bila shaka kunaongeza joto kwa mjadala wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Download App Yetu hapa chini, Bonyeza picha:-



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: