Rais John Magufuli amewataka viongozi wa madhehebu ya dini kuhubiri na kusisitiza amani ambayo ni msingi wa maendeleo.
Amesema hayo leo Aprili 8 katika misa ya kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Amani iliyofanyika katika parokia ya mtakatifu Theresia mjini humo.
Amenukuu maandiko matakatifu kutoka kwenye vitabu mbalimbali vya biblia yanayosisitiza amani.
Kuhusu maombi matatu yaliyotolewa na Padri Aloyce juu ya kuhamishwa Shule ya Msingi Naura ambayo ilianzishwa mwaka 1950 ikiitwa St Theresa School mali ya Kanisa hilo ambayo ilitaifishwa na Serikali mwaka 1967 alisema suala hilo lina changamoto kulipatia majibu ya haraka.
"Nikitoa tamko la kurejesha shule hii leo litasumbua sana kila mali zilizotaifishwa mwaka 1967 zitatakiwa kurejeshwa nami sitaki mgogoro huu," alisema Rais Magufuli
Alisema anaamini kila jambo lina wakati wake na waendelee kumuombea ili apate amani ya kutoa uamuzi sahihi.
Amesema hata suala la Shule ya Saint Jude inayotoa elimu bure kwa watoto wanaotoka kwenye Kaya zisizo na uwezo inayodaiwa kodi ya Sh6bilioni alisema hawezi kuingilia suala hilo kwakua lipo mahakamani na hataki kuonekana anavunja sheria.
Akizungumzia shughuli za maendeleo katika jiji la Arusha alisema kumekua na mafanikio makubwa katika huduma za elimu na afya.
Kwa upande wake Askofu Mkuu na Balozi wa Papa nchini, Maleck Schosist alitoa salamu zake na kumtaka Askofu Mkuu ,Amani kufanya kazi ya utume.
0 Post a Comment:
Post a Comment