Mchakato wa sheria mpya ya utalii sasa waanza


 



 Mchakato wa kupata sheria mpya ya sekta ya maliasili na utalii baada ya iliyopo kuonekana kuwa na upungufu na kuchelewesha maendeleo, umeanza.
Hayo yamebainika kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kuwakutanisha wadau wa sekta hiyo kurejea Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na kukusanya maoni ya upungufu na utekelezaji wake.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga alisema sera na miongozo inayoongoza sekta hiyo imepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyotokea huku akitolea mfano Serikali kujiondoa katika umiliki na uendeshaji wa huduma za kitalii na kuiachia sekta binafsi. “Si hivyo tu, sera ya awali haikuainisha vivutio vyote vya utalii zaidi ya hifadhi pekee ambazo tunatumia gharama kubwa kuzitangaza hadi nje,” alisema.
Alifafanua kuwa wanahitaji miongozo mipya itakayosimamia sekta hiyo ili kuondoa migongano ya kiutendaji katika taasisi zinazohusika ikiwamo ya wanyamapori, misitu na uwekezaji ili kuendeleza utalii na si kudidimiza.
Akifungua warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Aloyce Nzuki alisema wameamua kufanya mapitio ya sera hiyo kutokana na kasi ndogo ya maendeleo inayopatikana katika sekta hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Utalii, Wilbroad Chambulo alisema, awali sera hiyo haikuwa mbaya ila utekelezaji wake ulikuwa mgumu kutokana na wadau wa utalii kutofautiana na sera za chama tawala.     
  
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: