NMB yatatua changamoto ya JKCI



Changamoto ya kukosekana kwa sehemu ya kupumzikia wagonjwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) imetatuliwa baada ya Benki ya NMB kutengeza eneo hilo kwa ajili ya wagonjwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi eneo hilo mkurugenzi wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema itasaidia kupunguza msongamano wa watu wanaofika kusubiri matibabu.
"Uwezo wetu ni kupokea wagonjwa 100 lakini ukiangalia utamaduni wote mgonjwa anaweza kuja na wasindikizaji wawili hata watatu kwa hiyo watu wanakuwa wengi lakini wanakosa eneo la kukaa. Msaada huu ni mkubwa,"amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema ujenzi wa kituo hicho cha kusubiria ni sehemu ya mchango ambao benki hiyo umekuwa ukitoa kwa jamii.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: