Wakala wa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi (Cost), wamemlalamikia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuwa anakwamisha utendaji wao kutokana na kugoma kutoa taarifa za utendaji wao.
Akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa Coast, Mwenyekiti wa wakala hao Mhandisi Kazungu Magili alisema kuwa miongoni mwa kipimo cha utendaji uliotukuka ni pamoja na kuwa muwazi.
Alisema anaishangaa TBA licha ya kuwa taasisi ya umma bado haitoi ushirikiano wa kulifanikisha hilo. "Miongoni mwa majukumu tuliyopewa kikanuni na kisheria ni pamoja na kuhakikisha miradi ya ujenzi inajengwa kwa gharama stahiki" alisema Mhandisi Magili.
0 Post a Comment:
Post a Comment