Jeshi lasambazwa Brasilia kuzuia vurugu


25 Mei 2017

Waandamanaji nchini Brazili
Waandamanaji nchini Brazili
Rais wa Brazil Michel Temer ameyasambaza majeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia, baada ya waandamanaji kuanza kulichoma moto jengo la serikali na kuharibu mengine.
Maafisa wanasema hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya kudhibiti mambo, baada ya waandamanaji elfu 35 waliokuwa wakielekea mjini na kuongoza moja kwa moja katika bunge la nchi hiyo na katika makaazi ya Rais.
Wakijaribu kuwatawanya waandamanaji, Polisi wamefyatua mabomu ya machozi katika uwati wa watu.
Tuhuma za rushwa zinazomkabili rais wa nchi hiyo ndizo zilizosababisha mchafuko huo wa kisiasa.
Kuna wasiwasi kwamba kusambazwa kwa wanajeshi kudhibiti mambo kunaweza kuchochea zaidi vurugu.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: