Miili ya wanafunzi wa Lucky Vicent yaagwa


Haki miliki y
8 Mei 2017
Arusha, Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan , ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vicent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.
Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.
Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi.
Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini,walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika kote nchini.
Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.
Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.Katika kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Fred Matiang'i.
Ibada na Dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: