Arusha: Maelfu wahudhuria ibada ya kuaga miili ya wanafunzi wa Lucky Vicent


 8 Mei 2017

Manejewa yakiwa kwenye meza maalum
Maelfu ya watu leo wamejitokeza kuhudhuria ibada ya pamoja kuwaaga wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vicent waliofariki dunia ajalini Jumamosi asubuhi.
Mwandishi wa BBC aliyepo Arusha Aboubakar Famau anasema majeneza 35 yenye miili ya waliofariki yalifikishwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwa ibada ya mwisho ya kuwaaga waliofariki kabla ya kufanyika mazishi sehemu tofauti.
Shughuli nyingi mjini Arusha zilisimama leo na hata maduka na biashara zingine kufungwa huku watu wengi wakifika uwanjani kuhudhuria ibada hiyo.
Baadhi ya watu waliofika kuomboleza walipoteza fahamu hivyo kupewa huduma ya kwanza huku wengine wakikimbizwa hospitalini.
Makamu wa rais Bi Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wakuu serikali waliohudhuria ibada hiyo.
Amevitaka vyombo husika vihakikishe suala la usalama barabarani linapewa kipaumbele.
"Nawaasa madereva kuwa makini wawapo barabarani na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara," amesema.
Waziri wa elimu wa Kenya Dkt Fred Matiang'i, mmoja wa wageni kutoka nje ya Tanzania waliohudhuria ibada hiyo, amewapa pole Watanzania kwa msiba huo.
Manejewa yakiwa kwenye meza maalum
Image captionMajeneza yakiwa kwenye meza maalum
"Kenya itaendelea kuwa pamoja nanyi kwenye kipindi hiki kizito cha msiba huu mzito uliowafika. Msiba huu si wa Tanzania peke yake ni wa wote hata kwetu Kenya Rais Kenyatta na mkewe wanawapa pole sana na kuwaombea," amesema.
Rais Magufuli kupitia ujumbe kwenye Twitter, ameelezea, jinsi alivyopatwa na huzuni kutokana na ajali hiyo.
"Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha. Tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu," amesema.
Ujumbe wa Magufuli TwitterHaki miliki ya pichaTWITTER
Majenza yakitolewa kwenye lori
Image captionMajeneza yakitolewa kwenye lori na wanajeshi wa JWTZ
Wanafunzi hao wa darasa la saba walifariki dunia pamoja na walimu 2 na dereva wa gari la shule hiyo ya msingi ya Arusha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni.
Wanafunzi watatu walijeruhiwa.
Rais Magufuli, akituma salamu za rambirambi Jumamosi alisema „ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla."
"Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu."
Baadhi ya waliohudhuria ibada hiyo wamezidiwa na huzuni
Image captionBaadhi ya waliohudhuria ibada hiyo wamezidiwa na huzuni
Wakazi wamejitokeza kwa wingi
Image captionWakazi wamejitokeza kwa wingi

Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: