Waandamanaji zaidi wameuwawa Venezuela


  • 4 Mei 2017
Venezuela
Baadhi ya waandamanaji,Venezuela
Idadi ya vifo katika kipindi cha mwezi mmoja nchini Venezuela imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 30, idadi hiyo imeongezeka baada ya waandamanaji kupambana tena na polisi wa kuzuia ghasia siku ya jumatano.
Kumekuwa na Ripoti kuwa watu wengi wamejeruhiwa, baadhi yao wamejeruhiwa na mabomu ya petroli yaliyokuwa yanarushwa na vijana waliofunika nyuso zao mjini Caracas waliokuwa wakiandamana kuelekea kwenye eneo la Bunge la kitaifa.
Venezuela
Image captionMapigano dhidi ya Polisi na waandamanaji
Huku Polisi walijibu mapigo hayo kwa kuwatawanya kwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira.
Hata hivyo Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro ameukosoa upinzani na kusema kuwa anapambana kuilinda nchi dhidi ya ugaidi na kuwaambia wanaomuunga mkono kuwa ni juu yao kuamua mustakabali wa Nchi
Maduro amesema raia wa Venezuela wanapaswa kuchagua njia iwe ya vita au amani, kama wanataka vizuizi barabarani au wanataka uwakilishi kwenye Bunge.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: