Wanafunzi wa shule ya msingi wakutwa na bangi


29 Mei 2017



Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wanafunzi wa Shule ya Msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai kwa kukatatwa na bangi misokoto 59.
  • Watu wawili wamefariki katika matukio mawili tofauti ambao ni mwanamke na mwanafunzi.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issah alisema Mei 28, mwaka huu, majira ya saa 10:30 Kijiji cha Kyengia wilayani Siha mwanamke mmoja Ephrata Masaki(53), alipigwa na shoti ya umeme wakati akianua nguo.
Alisema nguo hizo zilikuwa zimeanikwa kwenye waya uliokuwa umegusana na waya wa umeme nyumbani kwake na kwamba waya huo ulikuwa umechubuka na kusababisha kifo chake.
Alisema Mei 28, mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni, Kata ya Soweto mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Sadia Kamote(39), mkazi wa Sanya juu, aligundua kufariki kwa mtoto wake wa darasa la kwanza.
Alisema mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Selemani Said(8) ni wa Shule ya Msingi Kilingi alifariki baada ya kuteleza kutoka kwenye jiwe na kusombwa na maji katika mto Karanga katika daraja la Mangia Shirimatunda.
“Mwanafunzi huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu huku wenzake aliokuwa akiogelea nao katika mto huo wenzake watatu kunusulika kifo,”alisema Kamanda Issah.
Alisema mwili wa marehemu Masaki umehifadhiwa katika hospitali ya Kibong’oto kwa taratibu za mazishi huku mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mawenzi.
Katika tukio lingine  Mei 28, mwaka huu, majira ya saa 10:30 katika kijiji cha kwa Sadala jeshi hilo liliwakamata wanafunzi wanne wakiwa na begi dogo jeusi na baada ya kuwapekuwa walikutwa na bangi.
“Tulipowahoji watoto hao walisema walipewa mzigo huo na mama aliyejulikana kwa jina la Francisca Limo(43) kwa lengo la kwenda kuuza na tayari tumeshawakamata watuhumiwa kwa mahojiano zaidi,”Kamanda Issah.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: