Mfalme wa Saudia amfuta kazi mrithi wake



21 Juni 2017

Mfalme Salman wa Saudia amemfuta kazi mrithi wake
Mfalme Salman
Mohammed Salman kushotoachukua mahala pake Mohammed Nayef
Mohammed Salman kushoto achukua mahala pake Mohammed Nayef
Mfalme Salman wa Saudia amebadilisha mkondo wa urithi na kumfanya mwanawe wa kiume Mohammed bin Salman kuwa mwanamfalme na kuwa wa kwanza kumrithi.
Aliyekuwa mwanamfalme Mohammed bin Nayef amepokonywa taji lake na kufutwa kazi kama waziri wa maswala ya ndani.
Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 ataendelea kuwa waziri wa ulinzi mbali na kuwa naibu waziri mkuu.
Mabadiliko hayo yalitangazwa katika misururu ya amri za kifalme.
Chombo cha habari cha Saudia kimesema kuwa mfalme ametaka raia wa taifa hilo kumtii mwanamfalme huyo mpya siku ya Jumatano.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: