20 Juni 2017
Mfano wa chanjo hiyo
Shirika la utafiti wa kisayansi kutoka nchini Netherlands limeanza kufanya majaribio kwa wanadamu ya chanjo ya kupunguza kiwango cha mafuta katika mwili wa mwanaadamu na kwamba endapo utafiti huo utafanikiwa; wana matumaini kuwa chanjo hiyo itakuwa na uwezo wa kuzuia magonjwa ya moyo.
Watafiti hao wameeleza kuwa majaribio yao waliyokwisha kuyafanya dhidi ya panya yanaonesha kwamba chanjo hiyo imefanikiwa kuzuia na kuacha kuimarisha amana ya mafuta katika mishipa ya damu.
Imearifiwa kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kufanya mfumo wa kinga ya mwili kukabiliana na mafuta yasiyohitajika kutoka katika damu.
WATU WENYE MIILI MIKUBWA KUWEZA KUUNGUZA MAFUTA
Wanasayansi hao wanaamini kuwa chanjo hiyo inaweza kutumika kama njia mbadala wa zilizokuwa za kupunguza mafuta , pamoja na kuwasaidia, mamilioni ya watu ulimwenguni kupambana na mafuta yasiyohitajika mwilini.
Inatarajiwa kuchukua takriban miaka sita ili vipimo hivyo kukamilika.
0 Post a Comment:
Post a Comment