Muhimbili yaboresha huduma, yapunguza gharama za wagonjwa kupelekwa India

Katibu Mkuu  Wizara ya Afya ya Malawi Dkt. Charles Mwansambo  ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ili kupata uzoefu wa namna Taasisi hiyo inavyotoa huduma za kibobezi (super specialist).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Alhamisi 22 Jijini Dar es Salaam Dkt. Mwansambo alisema ametembelea MOI ili kuona uwezekano wa kuwaleta wagonjwa wa Malawi kupata huduma za Kibingwa za Mifupa, Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu badala yakuwapeleka India.

” Nimefurahi kuona kuwa tuna huduma nzuri za kibingwa kwa jirani zetu wa Tanzania, hili ni jambo jema na litatupunguzia gharama za kuwapeleka wagonjwa India badala yake tunawaleta hapa MOI” alisema Dkt.Mwansambo.

Aidha, Dkt. Mwansambo alipata fursa ya kutembelea vyumba vya upasuaji vya MOI, vyumba vya wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU), wodi za watoto na wodi maalum za kisasa za kulipia.

Kutokana na mafanikio ya miundo mbinu ya kisasa yaliyopo MOI Dkt. Mwansambo ameonyesha dhamira ya dhati ya kuleta madaktari wanafunzi hapa  ili wapate ujuzi wa zaidi.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI  Mhandisi .Reginald Kimambo alimueleza Dkt. Mwansambo kwamba huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo zimebobea katika  Mifupa, Ajali, Upasuaji wa ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu pamoja na kutua mafunzo kwa madaktari bingwa wa COSESCA.

Ziara hii imekuja baada ya mkutano wa 65 wa Mawaziri wa  Afya wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Download App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: