Nkurunziza afika Tanzania ziara yake ya kwanza nje tangu 2015



20 Julai 2017

Nkurunziza na Magufuli
Magufuli na Nkurunziza
ais Nkurunziza akiwa na mwenyeji wake Rais John Magufuli baada ya kufika Ngara, kaskazini magharibi mwa Tanzania
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu kufeli kwa jaribio la kupindua serikali yake zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Amesafiri na mawaziri kadha kwenda nchini Tanzania, ambao imetoa makao kwa zaidi ya wakimbizi robo milioni kutoka Burundi.
Watu hao waliikimbia Burundi baada ya mzozo uliotokana na hatua ya Bw Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Nkurunziza alikuwa akihudhuria mkutano nchini Tanzania wakati jaribo hilo lilipofanyika mwezi Mei mwaka 2015.
Mamia ya watu wameuawa tangu mzozo huo uanze wengi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.
Haki miliki ya pichaAF
Haki miliki ya piANIA
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: