Askofu anayepinga ndoa za jinsia moja asusia mkutano Uingereza

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

3 Agosti 2017

Askofu anayepinga ndoa za jinsia moja asusia mkutano Uingereza
Mmoja wa viongozi wakuu wa kanisa la kianglikana nchini Uganda, amesema kuwa hatahudhuria mkutano unaokuja wa viongozi wa kanisa la Anglikana ambao utafanyika mwezi Oktoba nchini Uingereza, kwa sababu hakubaliani na wale ambao wameanza kukubali ndoa za jinsia moja.
Askofu mkuu wa Uganda Stanley Ntagali  hakuwa tayari kukutana na wale wanaokubaliana na kile alichokitaja kuwa ndoa zisizoambatana na mafunzo ya Biblia.
Alisema amefanya uamuzi huo baada ya kuomba ushauri kutoka kwa viongozi wengine nchini Uganda.
Wakatai wa mkutano uliopita wa viongozi wa dunia uliofanyika Januari mwaka 2016, Askofu Stanley Ntagali aliamua kuondoka mapema na kutisha kutorudi tena ikiwa hali hiyo haitarekebishwa.
Tangu wakati huo makanisa ya kianglikana ya Scotland na Canada yameunga mkono ndoa za jinsia moja.
NIJUZE HABARI KWA 0625 966 236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: