Watu 30 wafariki katika mlipuko mskitini Afghanistan

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

2 Agosti 2017

mskiti Afghanistan
Mlipuko umesababisha uharibifu katika mskiti huko Herat
Milipuko na risasi zilizofyetuliwa katika mji uliopo Afghanistan magharibi - Herat imesababisha vifo vya watu takriban 30 na kusababisha wengine wengi kujeruhiwa.
Msemaji wa polisi katika eneo hilo amesema shambulio hilo limetekelezwa na mlipuaji wa kujitoa muhanga.
Hakuna kundi linalodai kuhusika.
Shambulio dhidi ya Mskiti wa Jawadia limetokea saa mbili usiku wakati mamia ya waumini walipokuwa wanaswali swala ya jioni.
Mskiti huo upo katika eneo la mji wa Herat ulio na idadi kubwa ya wasilamu wa madhehebu ya Shia.
Afisa wa serikali ameiambia BBC kwamba mlipuaji wa kujitoa muhanga alifyetua risasi ndani ya mskiti kabla ya kujilipua.
Herat, mji uliopo karibu na mpaka na Iran, unatazamwa kuwa mojawapo ya miji ya amani Afghanistan.
Katika mwaka uliopita, kundi la Islamic State limelenga maeneo ya Shia katika sehemu nyingi nchini.
Siku ya Jumatatu kundi hilo limekiri kuhusika na shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya ubalozi wa Iraq katika mji mkuu Kabul.
NIJUZE HABARI KWA 0625 966 236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: