Emerson Mnangagwa kuapishwa Leo 24 Nov 2017

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.
Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa kaka uwanja michezo wa Harare.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .
Emmerson Mnangagwa akiwahutubia wafuasi wake mjini Harare, Zimbabwe. tarehe 22 Novemba, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionEmmerson Mnangagwa alirejea kama shujaa Zimbabwe nchini Zimbabwe Jumatano
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.
Kiatu cha muundo wa mambaHaki miliki ya pichaTWITTER /CAESARZVAI
Image captionRaia wa Zimbabwe akiwa amevalia kiatu cha muundo wa mamba, kama ishara ya kumuunga mkono rais mpya anayeapishwa Emmerson Mnangagwa anayejiita ''Mamba''.
Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa.
Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari.
Robert Mugabe na mkewe Grace tarehe 8 Novemba 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Mugabe alishutumiwa kwa kumuandaa mkewe Grace kuchukua wadhfa wa urais
Bwana Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu Jumapili, na haifahamiki wako wapi .
Alhamis , taarifa zilielezea kuwa Bwana Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa.
Televisheni ya taifa imesema kuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bwana Munangagwa.
Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare wenye viti 60,000- huku waandalizi wakiwataka waZimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo.
lhamisi Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini (MDC ) alitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kisiasa ili kuondoa masuala yaliyoweka madarakani kwa muda mrefu utawala wa Bwana.
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai
Image captionKiongozi wa chama cha upinzani cha Movement fo Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai
Bwana Munangagwa alikimbilia nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita- na kurejea nchini Jumatano wiki hii ambapo alipokelewa kama shujaa.
Bwana Mnangagwa aliahidi kubuni ajira ambapo baadhi wanakadiria kuwa 90% ya watu hawana ajira.
"Tunataka kukuza uchumi wetu, tunataka amani, tunataka kazi, kazi, kazi ," aliuambia umati wa watu uliomshangilia mjini Harare.
Jumatano chama tawala cha ZANU PF kilisema kitafanya mageuzi kuondoa sheria zilizomfanya Mugabe kuwepo madarakani kwa muda mrefu.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: