Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akabidhi Machine za Ultra Sound vituo na hospitali 10

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amevikabidhi vituo na hospitali 10 za Mkoa wa Dar es Salaam, Mashine za Ultra Sound za kisasa aina ya GE Vscan zenye thamani ya shilingi milioni 143 ikiwa ni kutambua mchango wa hospitali hizo katika kutoa huduma bora ya uzazi kwa mama na mtoto.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mashine hizo na zawadi nyingine kwa wahudumu wa afya Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ni jambo lenye kutia moyo kwa wahudumu wa afya kuendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuhakikisha uzazi salama ambapo vifo vya mama na mtoto vinapungua mkoani Dar es Salaam, kama sio kumalizika kabisa.
Amewataka wataalamu hao kuendeleza uadilifu na kuchapa kazi kwa kuwa mkoa wa Dar es Salaam, umejikita zaidi katika kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya bora, na wanaepukana na maradhi ambayo mara nyingi yamekuwa yakigharimu maisha ya watu wengi.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magemba amesema mashine hizo ambazo Mkuu wa Mkoa amekabidhi zitasaidia utambuzi mapema wa matatizo ya uzazi ambayo yanahitaji mama mjamzito kuwahishwa katika hospitali kubwa kwa msaada zaidi.
Kauli ya Mganga Mkuu imeenda sambamba na ya Mshauri Mkuu wa kiufundi wa mradi wa kujenga uwezo wa CCBRT Dk Brenda Sequeiras D’Mello, ambaye amesema mpango huo wa kuzipatia hospitali mashine za Ultrasound ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa miaka saba wa kuwajengea uwezo watumishi wa afya na kuboresha miundombinu ya afya.

Tuma habari picha kwa WhatsApp 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: