Papa Francis apiga marufuku uuzaji wa sigara Vatican

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

Licha ya sigara kuiletea mamilioni ya fedha Vatican ,papa Francis amesema kuwa hawezi kuruhusu binaadamu kuathiriwa kiafya

Papa  Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao.
Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.
Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei .
Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka.
Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.
Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.
''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.
''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.
Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa wakati alipokuwa kijana havuti sigara.
Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru.
>>>Tuma habari Picha WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: