Slaa ateuliwa kuwa balozi na Rais JPM

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Aliyekuwa Katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA ameteuliwa kuwa balozi na Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Katika taarifa ilitolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ,Gerson Msigwa, haijataja kituo chake cha kazi. Ila imeeleza "ataapishwa baada ya taratibu kukamilika"
Dokta Wilbord Slaa alikuwa kiongozi muandamizi wa upinzani nchini Tanzania.
Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka huo.
Slaa amekuwa katika siasa kwa zaidi ya miongo miwili na kabla ya hapo alikuwa padri wa kanisa katoliki.
•Tuma habari picha, video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: