Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Utafiti wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito.
Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto.
Watafiti wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawafai kuwa na tashwishi yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao.
Takriban mimba 225 nchini Uingereza huishia mtoto kuharibika na watafiti wa utafiti huo wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo wanawake wataendea kulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto.
Utafiti huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida na unathibitisha tafiti ndogo nchini New Zealnd na Australia.
Tuma habari picha WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: