Kiongozi Mkuu wa Upinzani Morgan Tsvangirai afariki dunia

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.
Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65, na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jioni ya Februar 14.
Katika kipindi cha uhai wake, maisha yake ya kazi yaligubikwa na harakati nyingi za kisiasa dhidi ya mpinzani wake Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Aliwahi kupigwa na kufungwa mara kadhaa.
Morgan Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000, na kuanza kutoa changamoto kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekaa madarakani muda mrefu.
Kufuatia kifo hicho Bwana Tsvangirai . MDC inaelekea kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: