Mamia ya Wachimba migodi wakwama mgodini Afrika ya Kusini

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Mamia ya Wachimba migodi wamekwama katika mgodi mmoja wa dhahabu ulioko eneo la mkoa wa Free State nchini A-Kusini.

Kikosi cha uwokoaji ktk kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Sibanye kimesema zaidi ya wachimba migodi 950 wamekwama chini ya mgodi wa dhahabu wa Beatrix ulioko mkoa wa Free State kilomita 300 Kusini Magharibi mwa Johannesburg .

Chanzo cha wachimba migodi hao kukwama ilitokana na radi kubwa iliopiga na umeme kukatika bada ya mvua kubwa kunyesha nyakati za usiku wakati wachimba migodi hao walipokua chini ya mgodi .

Mgodi huo unamilikiwa na kampuni ya Sibanye-Stillwater.

Msemaji wa kampuni James Wellsted amesema wachimbaji hao 64 wako salama na wanapata chakula na maji.

Alielezea kuwa umeme umerudishwa katika mgodi huo lakini umeme huo hautoshi kuwatoa wachimbaji hao ardhini.

Jumuiya ya wachimba migodi ya AMCU imetoa wito zizidishwe juhudi za uwokoaji kwa sababu baadhi ya wanachama wao wanaumwa na inabidi watumie dawa.

 Jumuiya hiyo inayongozwa na Joseph Matunjwa imesema migodi mingi ya A-Kusini ina mazingira mabaya ya kazi .

Kwa sasa familia za wachimba migodi hao wanaokaribia elfu moja zimekusanyika njee ya mgodi huo ili kujua hatima ya watu wao.

Habari zaidi=> www.zakacheka.blogspot.com

Injili=> www.zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: