Nicolas Niyibikora: Wanawake ni chanzo cha uovu, hakuna jema linaloweza Kutoka kwao

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Muhubiri mmoja wa Rwanda huenda akajapata mashakani mbele ya vyombo vya habari baada ya kuwaita wanawake ''chanzo cha uovu'' katika mahubiri ya redio.
Muhubiri huyo wa kanisa la Seventh Day Adventist Nicolas Niyibikora aliwambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu wakati wa matangazo ya idhaa ya redio ya Amazing Grace mwezi Januari akionya kuwa ''hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa wanawake''.
''Unaposoma Biblia , ni nani aliyeleta dhambi duniani''? Aliuliza akiongezea, ''sio mwanamume''.
Tayari mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneneo kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa , kulingana na gazeti la Rwanda la New Times.

Kundi la kutetea haki za wanawake liliwasilisha malalamishi yake katika tume ya udhibiti wa vyombo vya habari ambayo inatarajiwa kukutana ili kuzungumzia swala hilo wiki ijayo.
Afisa mkuu Emmanuel Mugisha aliambia gazeti la New Times kwamba kuna uwezekano idhaa hiyo italazimika kujieleza.
Kanisa la Seventh Day nchini Rwanda limefanya juhudi za kujitenga na Niyibikora, ambaye wanasema alipigwa marufuku kwa miaka mitano.
Kwa Injili Bofya hapa
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: