Sugu na Masonga waachiwa kwa dhamana....Hukumu Yao ni February 26

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga katika kesi inayowakabili ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Sugu na Masonga wamekaa mahabusu kwa muda wa siku 24 baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande wa  Jamhuri.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wawili baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.

Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo.

Hakimu Mteite amekubaliana  na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.

"Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana, na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: