Kata ya Isamilo: CCM yaongoza matokeo ya awali Kata

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Mgombea udiwani kata ya Isamilo jijini Mwanza (CCM), Nyamasiriri Marwa anaongoza katika matokeo ya awali yaliyobandikwa vituoni.


Mgombea wa Chadema, John Kisieri anafuatia katika matokeo hayo ya uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika leo Februari 17,2018, huku idadi ya wagombea waliojitokeza ikiwa ndogo.
Katika kituo cha Shule ya Msingi Lake 2 chenye wapiga kura 375 ni 80 pekee waliojitokeza kupiga kura.
Yafuatayo ni matokeo ya awali katika baadhi ya vituo na idadi ya kura walizopata wagombea kwenye mabano ni; Shule ya Msingi Lake 2, CCM (54) na Chadema (25).
Katika kituo cha Shule ya Msingi Lake 1, waliojiandikisha ni watu 375, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 59, kura halali zilikuwa 58, huku moja ikiharibika, CCM imepata kura 30 na Chadema (28).
Kituo cha Shule ya Msingi Maendeleo 1 waliojiandikisha walikuwa 315, waliopiga kura 63, kura halali ni 62 na moja imeharibika. CCM (40) na Chadema (22).
Kituo cha Shule ya Msingi Maendeleo 2 waliojiandikisha walikuwa 316, kura zilizopigwa ni 58 na kura halali ni 58. CCM (32), Chadema (25) na mgombea wa CUF, Hashim Omary (1).
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: