Mbunge Mary Nagu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya

Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu (CCM) na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo jana walikamatwa  na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya  kushindwa kuelewana kiutendaji.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa aliagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.

Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali

“Ni kweli tumemkamata na sababu kubwa ni kuhamasisha wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo na pia anawataka wananchi wasishirikiane na Mimi wakati anajua Mimi nasimama kama serikali” alisema DC  Sarah Msafiri.




Download App YETU hapa⬇⬇




Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: