Mwalimu aliyemkashfu Rais Magufuli aingia matatani

Mwalimu wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli  kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia.

Aidha amesema kuwa kufuatia hali hiyo tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi ili washughulikiwe.

Download App YETU hapa⬇⬇




Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: