Nabii awalabisha miguu waumini wake Nigeria

Nabii mmoja kutoka Nigeria (39), Andrew Ejimadu wa kanisa la Christ Freedom Ministries amezua gumzo mtandaoni baada ya ku-post picha zake katika mtandao wa Facebook wakati wa kuabudu mitandaoni.

Nabii huyo ameshangaza maelfu ya watu baada ya kuonyesha picha za waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake akidai kuwa kwa kufanya hivyo watapata baraka na miujiza.

Nabii huyo aliweka picha hizo katika ukurasa wake na kuandika.“Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.”

“Kitu cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” Andrew Ejimadu.

Mwaka 2016, Nabii Ejimadu alipamba vichwa vya habari na kushikiliwa na polisi nchini Zambia yeye na kaka yake, Cleopasa Ejimadu kwa kosa la kumbaka binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikwenda kwenye makazi yao kwa ajili ya uponyaji na kupata ushauri wa kiroho.


App YETU hapa⬇⬇




Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: