Wanawake DRC wanapigania haki zao kumiliki ardhi


Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoachwa na wazazi wao au waume zao.
Na hii inatokana na mila na desturi zao zinazomtambua mwanaume kama mrithi pekee wa Ardhi.
Wanaharakati wa haki za wanawake nchini humo wako katika jitihada za kuwaelimisha jamii kuhusiana na madhara ya mila hizo.
Wanaweke wanaoishi vijijini katika jimbo la Congo central hawana haki ya urithi mali au ardhi ya wazazi au waume zao.
Mila ya jimbo hilo inapinga kabisa kumpa mke urathi.
Licha ya kwamba marehemu babake na mume wake walimiliki hekta nyingi za ardhi, Anny mambweni haruhusiwi kurithi mali hiyo.
Image captionLicha ya kwamba marehemu babake na mume wake walimiliki hekta nyingi za ardhi, Anny mambweni haruhusiwi kurithi mali hiyo.
Katika shamba la mama Anny mambweni, anajaribu kuondosha majani shambani .
Mjane huyu wa miaka 48 ametupika sana, ana watoto watano.
Huku jasho likimtiririka usoni anaonekana akishughulika katika shamba lake - ardhi alioikopesha.
Licha ya kwamba marehemu babake na mume wake walimiliki hekta nyingi za ardhi, mila na desturi haimrusu kurithi mali hiyo.
Anny anasema ana haki kama ndugu zake wa kiume kurithi mali hiyo ilioachwana marehemu babake, lakini nduguzangu wakiume walikataa kumpa hata kipande cha ardhi.
"Eti mwanamke hana haki ya kupewa urithi. Tizama hapa, nimelazimika kuilipa ardhi hii ninayolima ilhali babangu aliacha pori kubwa na ardhi"
Women villagers in South Kivu, DRC
"Tizama, nateswa kabisa mimi na watoto wangu, nadhani mila kama hio ni mila ambayo inastahili kufutwa kwani haiku ambatana na sheria" anasema Anny.
Mkuu wa kijiji hicho bwana Zuanikibeni Bungalo anasema ni vigumu kwa mila kubadilishwa.
"Mwana mke atabaki kuwa mwanamke tu, unajuwa mwanamume ndio ataendesha kizazi na yeye tu ndiye anayestahili kupewa urithi wa jamaa, hatuwezi kukiuka mila yetu ata siku moja"amesema Bungalo.
Lakini sauti zimeanza kupazwa sasa ili kuukataa utamaduni huu.
Alphonsine Ponga ni mwanaharakati wa kutetea haki za akina mama katika kijiji cha Mbaza Ngungu.
Yeye pia alikuwa mwathirika wa utamaduni huu.
"Wanawake wengi hapa wanaogopa sana, hawapendi tufuatilie swali hilo, hilo ndio tatizo.
Nimewaeleza hio ni haki yetu, ni lazima tusimame, na kama umeona tatizo hilo nenda ukashtaki mahakamani".
Ponga ameeleza kwamba sheria ya Congo haina ubaguzi katika suala la urithi. Lakini katika hali kawaida , ni mila ndo imeendelea kukithiri zaidi ya sharia ya nchi hasa katika maeneo ya vijijini.

Download App YETU hapa⬇⬇


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: