Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alimtembelea mbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alimtembelea mbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu ambaye amelazwa katika hospitali ya Nairobi.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, makamu huyo alienda hospitalini humo muda mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta tarehe 28 Novemba.
Bwana Lissu amekuwa akipokea matibabu katika hospitali hiyo tangu mwezi Septemba 7 baada ya kupigwa risasu na watu wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma.
•Tuma habari picha, video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Makamu huyo wa rais ambaye aliandamana na kamishna wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana aliwasili katika hospitali hiyo mwendo wa saa kumi na moja.
Kwa mujibu wa gazeti hilo bi Samia ndio afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Tanzania kumtembelea bwana Lissu miezi mitatu baada ya shambulio.
Bwana Lisuu ambaye pia ni mkuu wa chama cha mawakili nchini Tanzania amekuwa akizozana na serikali ya rais Magufuli na alikamatwa mara sita mwaka huu pekee, akishtumiwa kwa kumtusi kiongozi huyo wa taifa mbali kuharibu usalama wa umma, miongoni mwa mashtaka mengine.
Ndiye kiranja wa bunge wa upinzani na wakili mkuu wa chama cha Chadema.
Alikamatwa mara ya mwisho mnamo mwezi Agosti baada ya kufichua kwamba ndege ilionunuliwa na kampuni ya ndege ya kitaifa Air Tanzania imekamatwa nchini Canada kutokana na deni la shilingi bilioni 83.
•Tuma habari picha, video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: