Lilikuwa tukio la kushangaza na kusisimua mwili. Mnyama wa majini mwenye vichwa vingi kwa jina hydra aliyewaogopesha watu wengi alijitokeza mbele ya Heracles-mwana wa mungu wa Ugiriki Zeus.
Lakini Heracles alikuwa na mpango mahsusi. Mapema aligundua kwamba hydra atamea kichwa chengine anapokatwa- hivyobasi akaamua kutafuta usaidizi kutoka kwa mpwa wake Lolaus.
Ni wazi kwamba waligundua matokeo hayo yasio ya kawaida katoka miili yao. Wakati Heracles alipowavamia wanyama hao, mpwa wake Lolaus alijitokeza na kukata shingo zao na kuzuia vichwa vya mnyama huyo kumea upya
Wakati huo wote Mnyama Hydra alitoa sauti kali na kusongea huku damu yake na hewa aliyokua akitoa ikitishia kumuangamiza shujaa wa Ugiriki.
Lakini Heracles alifanikiwa kukikata kichwa cha hayawani huyo.
Hydra ni mnyama aliyekuwa na sifa za kuwa na zaidi ya vichwa 50 lakini picha nyingi zilimuonyesha akiwa na vichwa vichache zaidi ya vilivyodaiwa.
Lakini wazo hili la mnyama mmoja kuwa na zaidi ya kichwa kimoja lilitoka wapi?
Je Wagiriki walikuwa na wazo la hayawani aliyekuwa na vichwa vingi. Wanasayansi walionyesha visa visivyokuwa vya kawaida vya wanyama wenye vichwa viwili kwa miaka mingi.
Na hivi karibuni mwanabaiolojia endelevu Arkhat Abhzanov katika taasisi ya Imperial College mjini London, ameona mifano mingi ya wanyama wenye vichwa viwili katika mahabara yake na kubaini mabadiliko yanayoweza kusababisha hilo.
Ni kweli kwamba kadri ya muda unavyosonga wanyama wenye vichwa viwili na hata vitatu wanapatikana misituni ama katika hifadhi.
Cha kushangaza ni kwamba swala hili linalojulikana kama polycephaly-halifanyiki tu kwa wanyama wa aina moja .Kwa mfano samaki .
Mwaka 2013 kijusi cha papa mwenye vichwa viwilli kilipatikana katika Ghuba ya Mexico.
Mwaka uliofuata , kisa chengine kama hicho kilipatikana katika wanyama wanaoishi baharini baada ya pomboo mwenye vichwa viwili kupatikana katika fukwe za bahari za Uturuki.
Mifano yote miwili inaonekana kuwa ya pcha walioshikana-kutokana na yai lisilogawanyika kabisa . Uso hutengezwa na jeni.
Orodha ya mifano ya wanyama ni ndefu mno ikiwemo makobe, nyoka na hata paka.
Haya sio matokeo ya siku hizi kwani wanasayansi wamewahi kupata mabaki ya viinitete vyenye vichwa viwili kutoka miaka milioni iliopita.
Kama Abzhanov anavyoelezea kuna sababu kadhaa ambazo husababisha mnyama kuwa na zaidi ya kichwa kimoja ama nyuso zaidi ya moja.
Wanyama wenye uti wa mgongo ama wasio na sehemu hio wote hufaidika kwa kuwa na vichwa vingi lakini hutoka kwa vizazi tofauti .
Hii ndio maana viungo kama vile macho, masikio, pua na mdomo hupatikana hapo. Utengezaji wa uso unatokana na jeni za mnyama mwenyewe. Na jeni moja huwa na athari kubwa hususan katika upana wa uso.
Ni wanyama wenye uti wa mgongo walio na jeni hiyo ya SHH.
Azbhanov anasema kuwa wakati nungunungu anayeendelea kukuwa anapodhoofishwa basi kichwa chake huwa chembamba na mara nyengine kinashindwa kukuwa na kusababisha wanyama kuzaliwa na jicho moja na kichwa kidogo.
Kiini kinachojulikana kusababisha kasoro hiyo katika kondoo hujulikana kama "cyclopamine".
Hupatikana katika mafuta ya mahindi kwa mfano na huliwa sana na wanawake wajawazito. Unapochukua kundi la seli hizo na kuliweka katika kiinitete cha chura atakuwa na vichwa viwili.
Unapoongeza jeni za SHH na kuwa nyingi ,uso unakuwa mpana hadi vichwa viwili vinajitokeza.
''Visa kama hivyo sio vya kawaida lakini huripotiwa miongoni mwa wanyama wanaofugwa nyumbani pamoja na wale wa msituni'', kulingana na Abzhanov.
Kimaumbile, mnyama mwenye nyuso mbili hujitokeza na sio vichwa viwili. Kwa wanyama walio na shingo mbili tofauti zinazomea kutoka kwa mwili mmoja ,Abzhanov aligundua tatizo jingine ambalo hujitokeza mapema katika ukuaji wa kiinitete.
Kichwa ni kama kiungo chengine cha mwili na hukua kutokana na kundi moja la seli ,mapema wakati kiinitete kinapokuwa.
Unapochukua kundi moja la seli na kuliweka katika kiinitete cha chura , chura hicho kitakuwa na vichwa viwili.
Hilo ni wazi kwamba kundi hilo la seli hutoa ishara ambayo huambia mnyama huyo kutoa kichwa.
Hili ndilo linalofanyika katika kisa cha pacha walioshikana lakini Abzhanov amegundua hilo likifanyika katika maabara.
Azbhanov anadai kwamba sababu moja ni hali ya joto. Yeye na wenzake walichukua mayai yaliorutubishwa kutoka kwa shamba la kuku.
Viinitete hivyo baadaye huchunguzwa katika maabara . Lakini katika wakati wa joto kundi hilo la watafiti liliweza kubaini tatizo lisilo la kawaia .
''Wakati joto linapofikia nyuzi 30, mayai hayo huo na kiwango cha juu cha kasoro , ikiwemo kiinitete chenye vichwa viwili'', alisema.
La kushangaza ni kwamba tatizo hilo limeweza kutokea kwengineko, mmoja wa wanabiolojia hao kwa mfano alibaini kwamba viwango vya juu vya joto katika maji husababisha ukuaji wa kiinitete chenye vichwa viwili.
Haijulikani ni kwa nini hilo hutokea , lakini utafiti zaidi unafanywa ili kubaini ushawishi wa joto katika kusababisha kasoro kwa wanyama.
0 Post a Comment:
Post a Comment