Mpanda milima maarufu duniani 'Ueli Steck' afariki Everest


  • 1 Mei 2017
Ueli Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashini ya Uswiswi, alikufa kwenye ajali akipanga mlima
 Ueli Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashini ya Uswiswi, alikufa kwenye ajali akipanga mlima
Mmoja wa wapanda milima maarufu zaidi duniani Ueli Steck, amefariki katika Mlima wa Everest.
Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashini ya Uswiswi, alifariki kwenye ajali, alipokuwa akijaribu kujizoesha kupanda mlima huo kwa kupita njia mpya na bila ya kutumia gesi ya oxygen.
Steck, alikuwa na umri wa miaka 40, na ameshinda tuzo kadha huku akijulikana kwa kukwea milima kwa kasi.
Mwili wake umetolewa mlima Everest na kupelekwa mji mkuu wa Nepal, Kathmandu.
Ueli Steck aliweka reko mpya wa kukwea milima kwa kasi na kutumia njia mpya.
Pia alichangia katika mchezo huo kupata mashabiki wapya kutokana na filamu kumhusu zilizotengezwa.
Mwaka 2015 alipanda moja ya kuta maarufu zaidi duniani unaofahamika kama North Face of the Eige, kwa muda wa saa 2 na dakika 47, jaribio lililowachukua watangulizi wake siku kadha kukamilisha.
Ueli Steck amefanikiwa kupanga mlima Everest awali bila hewa ya oxygenHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUeli Steck amefanikiwa kupanga mlima Everest awali bila hewa ya oxygen
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: