Mkurungenzi wa runinga ya Iran auawa Uturuki


  • 1 Mei 2017
Saeed Karimian alikuwa ndani ya gari pamoja na mshirika wake wa kibiashara
Saeed Karimian alikuwa ndani ya gari pamoja na mshirika wake wa kibiashara
Mkurugenzi mkuu wa kampuni moja ya runinga ya Iran ameuwawa kwa kupigwa risasi akiwa mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.
Saeed Karimian alikuwa ndani ya gari pamoja na mshirika wake wa kibiashara wakati watu waliokuwa na bunduki huku wakijifunika nyuso zao walishambulia gari lao.
Wote wawili waliuawa.
Runinga ya bwana Karimian, Gem TV, huwa inapeperusha vipindi vya mataifa ya magharibi na mataifa mengine kwa lugha ya kipersia.
Amekuwa akishutumiwa kwamba anaeneza taarifa za kupotosha dhidi ya Iran, huku mwanahabari wa BBC akisema kuna baadhi ya watu wanaosema kwamba aliuwawa na maafisa wa iran.
Runinga ya bwana Karimian, Gem TV, huwa inapeperusha vipindi vya mataifa ya magharibi kwa lugha ya kipersia.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRuninga ya bwana Karimian, Gem TV, huwa inapeperusha vipindi vya mataifa ya magharibi kwa lugha ya kipersia.



 Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com/ www.zakacheka.simplesite.com +255 625966236

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: