Polepole: Nape alikengeuka


Katibu wa Itikadi na Uenezi (KIU) wa CCM,

Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni.
Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.
Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
“Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa.  Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema Nape.
Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa amekengeuka.
“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji  Polepole.





                           Comment, like and share

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: