Castro ashuhudia maadhimisho ya mwisho ya wafanyakazi Cuba


  • 2 Mei 2017
Raul Castro ametangaza kuondoka madarakani mwezi Februari mwakani
Image captionRaul Castro ametangaza kuondoka madarakani mwezi Februari mwakani
Mamilioni ya raia wa Cuba wameshiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika sehemu maarufu ya iitwayo Havana Square na nyinginezo ikiwa ni ya kwanza tokea kifo cha Rais wa zamani Fidel Castro na ya mwisho kabla ya Rais wa sasa Raul Castro kuondoka madarakani.
Familia ya Castro imekua madarakani tokea mwaka 1976
Image captionFamilia ya Castro imekua madarakani tokea mwaka 1976
Maadhimisho hayo yaliambatana na kuimba nyimbo mbalimbali, kubeba bendera, pamoja na kuvaa nguo zenye rangi ya bendera ya nchi.
Raul Castro anatarajia kuachia ngazi mwezi Februari mwakani, huku ikitazamiwa kuwa mwisho wa kizazi hicho madarakani.
Haijawekwa wazi ni nani atakayechukua nafasi hiyo.
 Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com/ www.zakacheka.simplesite.com +255 625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: