Waandishi wa habari wagoma wakipinga kupunguzwa ajira Australia

Waandishi wa habari wagoma kupinga kupunguzwa ajira Australia

  • 3 Mei 2017
Siku ya Jumatano Fairfax ilisema kuwa itaawachisha kazi wafanyakazi 125
Siku ya Jumatano Fairfax ilisema kuwa itaawachisha kazi wafanyakazi 125
Waandishi wa habari katika shirika la habari la Fairfax Media, moja ya wachapishaji wakubwa zaidi nchini Australia wamefanya mgomo kwa wiki moja wakilalamikia kupunguzwa kwa nafasi za ajira.
Siku ya Jumatano Fairfax ilisema kuwa itaawachisha kazi wafanyakazi 125 ambayo ni robo ya wafanyakazi wa chumba cha habari.
Kujibu hilo sasa wafanyakazi watagoma hadi baada kusomwa kwa bajeti wiki ijayo ambayo ni siku kubwa kwa vyombo vya habari.
Sawa na mashirika mengine ya habari kote dunaini, Fairfax inakumbwa na changamoto za kushuka kwa mauzo ya magazeti yake na kupungua na pesa zinazotokana na matangazo.
Matawi ya Fairfax's ni pamoja na Sydney Morning Herald, The Age la mjini Melbourne na Australian Financial ReviewHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMatawi ya Fairfax's ni pamoja na Sydney Morning Herald, The Age la mjini Melbourne na Australian Financial Review
Matawi ya Fairfax's ni pamoja na Sydney Morning Herald, The Age la mjini Melbourne na Australian Financial Review
Tangazo hilo la kupunguza wafanyakazi limetangazwa sawa na mipango ya kuanza kutumia waandishi wa habari wa kujitegemea.
Muungano wa vyombo vya habari nchini Australia ambao unawaakilisha waandishi wa habari nchini humo, umekosoa vikali mipango hiyo ya kupunguza wafanyakazi kama hatua mbaya.
Fairfax ndiye mshindani mkubwa wa shirika la Rupert Murdoch la News Corp Australia, amablo nalo linakumbwa na matatizo ya kifedha na ambalo limetangaza kupunguza wafanyakazi.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: