Waziri mwenye umri mdogo zaidi Somalia auawa


  • 4 Mei 2017
Abas Abdullahi alikuwa katika gari hili na aliuawa akitokea katika shughuli zake
Abas Abdullahi alikuwa katika gari hili na aliuawa akitokea katika shughuli zake
Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu.
Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais.
Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia.
Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland.
Image captionAbas Abdullahi hakuwa na uzoefu katika siasa lakini alipendwa na wengi
Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri.
Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.
Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: