Kifo cha Otto Warmbier: Trump aishutumu Korea Kaskazini



20 Juni 2017

Rais Donald Trump amechukizwa na utawala wa Korea kaskazini kufuatia kifo cha Otto Warmbier
Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump ameutaja utawala wa taifa la Korea Kaskazini kuwa wa kikatili kufuatia kifo cha mwanafunzi mmoja wa Marekani ambaye alikuwa amefungwa jela kwa zaidi ya miezi 15 nchini humo.
Korea Kaskazini ilimrudisha nyumbani Marekani, Otto Warmbier mwenye umri wa miaka 22 wiki iliopita ikisema kuwa alikuwa hana fahamu kwa kipindi cha mwaka mmoja na kwamba ilikuwa ikimsaidia kibinaadamu.
Wazazi wake wanasema kuwa aliteswa vibaya.
Bwana Warmbier ambaye alifungwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwa hoteli moja hakuweza kupata fahamu tena.

Otto Warmbier alipokamatwa baada ya kujaribu kuiba bango la propaganda
Otto Warmbier alipokamatwa baada ya kujaribu kuiba bango la propaganda

Haki miliki ya picha
Bwana Trump alisema kuwa kifo cha Warmbier kimeimarisha mipango ya utawala wake wa kutaka kuwatetea wengine kupata majanga kama hayo katika mikono ya mataifa yasioheshimu sheria.
''Marekani kwa mara nyengine inashutumu ukatili wa utawala wa Korea kaskazini huku tukimkumbuka mwathiriwa wa hivi karibuni''.
Wazazi wa Warmbier Fred na Cindy walisema katika taarifa kwamba mwanao alifariki siku ya Jumatatu katika hospitali ya Cincinnati ambapo alikuwa akipewa matibabu.
Wanasema kwamba wakati Otto aliporudi Cincinnati alikuwa hawezi kuzungumza na hakuweza kuona.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: