Sherehe ya kula nyama ya mbwa yafanyika China


21 Juni 2017

Baadhi ya wauza nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin
Baadhi ya wauza nyama ya mbwa katika sherehe ya YullinWateja wa nyama ya mbwa wakibugia vipande vya nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin ya mwaka uliopita

Wateja wa nyama ya mbwa wakibugia vipande vya nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin ya mwaka uliopita
Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu.
Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.
Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.
Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa.
Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.

Haki miliki ya p

Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.
Mwanaharakati mmoja aliliambia shirika la  BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa.
Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangiwa kuchinjwa.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: