Mwanamume aliyeingizwa kwenye jeneza Afrika Kusini atoa ushahidi Mahakamani

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

3 Agosti 2017
Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.
Mwanamume mmoja mweusi ambaye anadaiwa kulazimishwa kuingia ndani ya jeneza na wanaume wawili wazungu ambao walitishia kumchoma akiwa hai ametoa ushahidi mbele ya mahakama nchini Afrika Kusini.
Victor Mlotshwa aliangua kilio kwenye mahakama kuu ya Middleburg wakati alikumbuka kisa hicho cha mwezi Agosti mwaka uliopita.
Mahakama ilicheza video ya kisa hicho ambapo bwana Mlotshwa anaweza kusokika akilia na kuomba washambuliaji kumsamehe.
Haki miliki ya picha
Anadai kuwa wakulima Theo Jackson na Willem Oosthuizen walimfunga kwa nyaya wakampiga na kutishia kumpiga risasi.
Theo Jackson na Willem Oosthuizen
Theo Jackson na Willem Oosthuizen
Washukiwa hao wawili wanakana hilo wakidai kuwa walimpata bwana Mlotswa akiiba nyaya.
Wanasema kuwa lengi lao lilikuwa ni la kumfunza adabu. Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.
NIJUZE HABARI KWA 0625 966 236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: