Punda watumiwa kuiba magari kutoka Afrika Kusini

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

2 Agosti 2017

A pace of donkeys are photographed next to a stolen vehicle
Punda watumiwa kuiba magari kutoka Afrika kusini kwenda Zimbabwe
Polisi nchini Afrika Kusini wametibua jaribio la kulisafirisha gari moja la kifahari lililokuwa limeibwa kwenda nchini Zimbabwe kwa kutumia punda kupitia mto Limpopo.
Washukiwa walitoroka kwenda vichakani kueleka upande wa zimbabwe baada ya jitihada zao za kulikwamua gari hilo kutoka kwenye mchanga kushindikana.
Disemba iliyopita gari lililokuwa limeibwa kutoka mjini Durban lilipatikana mtuo huo huo likiwa limefungiwa kwa kutumia kamba kwa kundi la punda.
Polisi wanachunguza ikiwa kuna genge linalohusika na wizi huo.
Mto Limpopo ndio mpaka kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe na ni maarufu kama njia wanayopitia wahamiaji haramu kati ya nchi hizo mbili, lakinia ataraiga za mto huo kutumia kupitisha magari yaliyobwa bana za kushagza.
NIJUZE HABARI KWA 0625 966 236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: