10 Sep 2017
Kimbunga Irma kimepiga visiwa vilivyo kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani kikiwa katika kiwango cha nne, kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa.
Kimbuga hicho kinatarajiwa kupiga visiwa vilivyo nyanda za chini na upepo wa kasi ya hadi kilomita 209 kwa saa kabla ya kuelekea kaskazini magharibi kwa ghuba ya Florida.
Zaidi ya watu milioni 6.3 waliambiwa waondoke Florida, huko onyo likitolewa kuwa kubunga hicho kinaweza kuwa tisho kwa maisha.
Irma tayari kimeharibu eneo ya Caribbean ambapo takribana watu 25 wameuawa.
Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili.
Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani.
Tampa inasemekana kuwa ni mji ulioko katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani, hasa kuhusiana na hatari ya kugongwa mara kwa mara na vimbunga.
Pia wakuu jimbo la Florida wametangaza hali ya tahadhari ya kutotoka nje, katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo, ukiwemo mji wa Miami
Tufuate facebook: zakacheka.blogspot.com
0 Post a Comment:
Post a Comment