17 Sep 2017
Maandamano baada ya polisi mzungu kuondolewa mashtaka ya kumuua mtu mweusi
Maandamano mapya yametokea katika mji wa St Louis nchini Marekani, ambapo polisi mzungu wa zamani alipatwa kutokuwa na hatia kwa kumuua mtu mweusi mwaka 2011.
Mamia ya watu waliandaanama katika mji wa Missouri kwa siku ya pili wakisema kuwa maisha ya weusi yana maana.
Zaidi ya waandamanaji 33 walikamatwa na polisi 11 kujeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Ijumaa usiku.
Polisi huyo Jason Stockley 36, aliondolewa mashtaka ya kumuua Antony Lamar Smitjh 24.
Jumamosi jioni, polis walitokea wakati waandamanaji walikusanyika katika mji wa St Louis.
Maandamano baada ya polisi mzungu kuondolewa mashtaka ya kumuua mtu mweusi
Bwana Smith alikuwa baba na alikuwa afunge ndoa wakati aliuawa tarehe 20 Desemba mwaka 2011.
Bwana Stockley na mwenzake walisema waliamini kuwa Bw Smith alikuwa akishriki katika kitendo kinachohusu madawa ya kulevya nje ya mkahawa.
Bwana Smith alikuwa baba na alikuwa afunge ndoa wakati aliuawa tarehe 20 Desemba mwaka 2011.
Baada ya kumfuata kwa kasi kwa muda wa dakika tatu, Bw Stockley alimuambia mwenzake ambaye alikuwa akiendesha gari aligonge gari la Smith.
Bwa Stockley kisha akakimbia kwenda kwa dirisha la gari la Smith na kumfytulia risasi mara tano.
Polisi Jason Stockley
0 Post a Comment:
Post a Comment