Utajiri wa Kristo usiopimika

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>


Ni muhimu kufahamu utajiri wa dunia hii unapimika. Ndiyo maana anafahamika tajiri wa kwanza duniani, Afrika na hata nchini Tanzania. Utajiri huu hutokana fedha na mali  alizonazo mtu.

Utajiri wa Kristo usiopimika anakuwa nao mtu aliyeokoka tu. Hii ni siri ambayo Paulo Mtume aliihubiri kwa mataifa 
( WAEFESO 3:8).

Hata kama mtu ni tajiri namba moja duniani, kama hana huu utajiri wa Kristo usiopimika, yaani hajaokoka, bado ni maskini. 

Yesu Kristo mwenyewe ndiye anayewaita hawa wenye dhambi maskini na ndiyo maana wanahitaji kuhubiriwa injili ili watubu dhambi zao na kumwamini na kisha kuokoka. (LUKA 4:18). Huu ndiyo utajiri aliouzungumzia Baba Askofu Kakobe na ambao ataendelea kuuzungumzia.

Lakini kwa mshangao mkubwa, TRA, siyo tu kwa mahubiri haya walimpekua, bali pia walitangaza hadharani kiasi cha fedha kilichoko kwenye akaunti ya kanisa. Je, kulingana na "Job description ya TRA" kuweka hadharani akaunti za makanisa ni sehemu ya kazi yao? Je, ni kweli Askofu Kakobe aliomba radhi ETI kwa kuzungumuza maneno ya kejeli? TRA wanapaswa kufahamu waongo wote sehemu yao ni katika ziwa la moto (UFUNUO WA YOHANA 21:8). 

Ndugu zangu, mtu amewekewa kufa mara moja na baada ya hapo ni hukumu ( WAEBRANIA 9:27). 

Tusidanganyike, hakuna sala yo yote ya kuwaombea wafu itakayoleta badiliko kwamba eti mtu aliyehukumiwa kwends motoni watu waombe kisha atolewe huko na kupelekwa mbinguni. Ingekuwa hivyo, yule tajiri aliye motoni hata sasa asingeomba mtu atumwe kutoka kwa wafu akawahubiri ndugu zake ambao walikuwa duniani ili watubu wasiende pale alipo (LUKA 16:19-31). Tujifunze kumwamini na kumtegemea yeye na siyo wanadamu wenzetu. Mungu mwenyewe anasema ye yote anayemwamini mwanadamu mwenzake amelaaniwa (Yeremia 17:5). Mwenye masikio na asikie.

By Santy Kimaro, FGBF Dar
Kwa Injili Bofya hapa
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: