Makamu wa Rais akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bill Gates Foundation

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw. Rodger Voorhies kwenye makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma 23 Machi, 2018 .

Makamu wa Rais amesema amezungumza mambo mengi na Bw. Rodger hasa kwenye masuala ya afya, uwezeshaji wanawake kiuchumi, kuwatoa kwenye kilimo cha sasa na kuwaingiza kwenye kilimo biashara lakini pia kuongeza thamani ya mazao na mambo ya masoko.

Makamu wa Rais alisema wamezungumza namna ya kuwarasimisha wanawake wa vijijini na wanawake wakulima ikiwa pamoja na uwezekano wa wanawake vijijini kuweza kupata mikopo.

Aidha Makamu wa Rais alizungumzia suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama haswa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo mara kwa mara kumekuwa na milipuko ya magojwa ya kipindu pindu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw. Rodger Voorhies alisema wamekuja kwa Makamu wa Rais kuzungumza juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo hapa nchini haswa katika masuala ya Kilimo na Afya na Mkakati Mpya wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Aidha wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua kubwa ambayo wamepiga katika kuwajumuisha wanawake katika masuala yanayohusu Fedha.

Mwisho, Mkurugenzi huyo ameahidi ushirikiano mkubwa kwa Serikali ya Tanzania katika kutekelezaji wa miradi ya taasisi yao.

Download App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: