Islamic State wameulipua msikiti mkuu wa Al-Nuri wa kihistoria Iraq



 22 Juni 2017

Iraq
Msikiti wa Al-Nuri kabla ya kulipuliwa
Jeshi nchini Iraq limethibitisha kwamba wanamgambo wa dola ya kiislam Islamic State wameulipua msikiti mkuu wa Al-Nuri ulioko mjini Mosul .
Msikiti huo unaaminika ndimo kiongozi wa wanamgambo wa IS Abu Bakr al-Baghdadi alitoa hotuba yake miaka mitatu iliyopita wakati alipokuwa akitangaza "ukhalifa" mpya.
Wakati hayo yakijiri, wanamgambo hao wa IS wao wanadai kwamba ndege za jeshi la Marekani ndiyo zilizo zilizousambaratisha msikiti huo.
Mapema leo, Kamanda wa majeshi ya Iraq aliiambia BBC kwamba walikuwa mita kadhaa kutoka msikitini hapo, walipokuwa katika harakati zao za kusonga mbele kwenye mapambano lengo likiwa ni kuteka ngome kuu ya wanamgambo hao wa kiislam wa Is nchini Iraq.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: